Monday, November 12, 2012

MARIAMU KHAMISI AFARIKI DUNIA.


MWIMBAJI wa nyota wa taarabu nchini Mariamu khamisi ametutoka dunia usiku wa kuamkia leo,taarifa ambazo nilizipata kupitia kwa msanii mwenzie thabit abduli nikwamba mariamu amefariki uzazi katika hospitali ya muhimbili jijini daa es salam, na pia nilibahatika kupata taarifa kupitia kwa shogaake mpenzi ambae anaitwa Suhaiya khasani  yeye ni rafiki ake wa karibu sana na baada ya Mariamu kuumwa uchungu waliongozana wote na kwenda hospitali ya BALISINA walipo fika madokta wakamwambia njia ni ndogo aende hospitali yaMWANANYAMARA na hapo walipo fika pia madokta waka mwambia aende hospitali ya MUHIMBILI huko ndiko alipo patwa na umauti baada ya kufanyia operesheni na kujaaliwa kupata mtoto wa kike na nayeye kutokuamka kabisa, Marimu khamisi kabla ya kua katika kundi la TOTI alikua akiimbia kundi la FIVE STAA,aliwahi kuimba nyimbo nyngi,ULIWEZI BIFU <SIDHURIKI NA LAWAMA NK.
Baada ya kijiunga na kundi la TOT yalisemwa mengi sana juu yake lkn yeye mwenyewe kumbwa alilo sema'nanukuu " hajapotea njia na ameamua kwa hiyari yake mwenyewe na hajashawishiwa,na lengo la kuhamia huko ni kwaajili ya maslhi na kijitafutia maish,katika picha ambayo unaiona hapo juu mariamu ni wa kwanza kabisa,duniani tumekuja kutembe tu kila mtu ataonja mauti INNALILAHI WAINNA IAIHI RAJGHUUN>

Friday, October 19, 2012

LULU AIBUKA NA SINGLE YAKE

Ni msanii mpya Lakini pia anafanya shughuli za utangazaji kupitia Safari Fm Mtwara Jina Halisi Zakia Lulu Jama Na Jina La Kisanii Ni ELLE,Ngoma yake hii mpya na ya Kwanza amemshirikisha kijana pia anechipukia kimuziki toka Mtwara Pia na Ngoma yenyewe hii imefanyika Mkoani Mtwara Na Producer Geoff Master.......Ni Zouk Moja Nzuri Na Tam Sana....Pata Muda Wa Kusikiliza Uone Utofauti Amezaliwa August 31 Na ukitaka mengi zaidi kujua kutoka kwake mcheki katika Facebook (Lulu Jama)......

FURAHA YANGU YAGEUKA ZAWADI BABY J

WASANII WATATU AKIWEMO ALPHA KUTOKA JUPITER RECORDS, JOBFIRE KUTOKA MK
RECORDS NA ABRAMY KUTOKA APRISE MUSIC WAMEFANYA REMIX YA WIMBO WA BABY J FURAHA YANGU KAMA ZAWADI KWA MWANADADA HUYO AMBAYE KWA SASA ANATARAJIA KUINGIA KATIKA MAISHA YA NDOA.

WAMESEMA KWAMBA KUTOKANA NA KUZIKUBALI SANA KAZI ZA MWANADADA HUYO ANAYEFANYA POA KTK GAME LA MUZIKI WA KIZAZI
KIPYA WAMEPENDA KUMZAWADIA WIMBO HUO WA FURAHA YANGU KAMA KUMPONGEZA KWA MAAMUZI YA BUSARA ALIYOYAFANYA KWA KUAMUA KUWA TAYARI KUINGIA KATIKA HARAKATI ZA KUELEKEA KWENYE MAISHA YA MUME NA MKE JAMBO AMBALO NI LA BUSARA NA HEKIMA KTK MAISHA. WANAMTAKIA KILA LA KHERI MWANADADA JAMILA ABDALLAH A.K.A BABY J KTK SAFARI YAKE YA KUELEKEA KTK MAISHA YA NDOA. TUNAMPENDA SANA NA KUMJALI DADA YETU NA PIA TWAZIPENDA KAZI ZAKE.

MZIGO MPYA AACHIA QUEEN DARLEEN

Mwanadada Queen Darleen aachia Ngoma Mpya inaitwa KOKORO......Imefanywa Na Producer Tuddy Thomas.....Video Inafanywa Wiki Hii Na Adam Juma (Visual Lab Next Level)
Hii Ni Ngoma Yake Ya 5 Tokea Ameanza Kufanya Mziki Mwaka 2000 Ya Kwanza Ilikuwa Wajua Ft. Alikiba, Ya Pili Ilikuwa Cheza Nami Ft. Kgt, Ya 3 Ilikuwa Ilikuwa Kupendapenda Ft. Sho daddy, Ya 4 Ilikuwa Maneno Maneno Ft. Dully Sykes Na Ilifanikiwa Kuchukua Tuzo Ya Best Dancehall/Ragga Kupitia Kili Awardz 2011-2012 Na Kokoro Ndio Single Ya 5.

Thursday, September 6, 2012

MAANDALIZI YA SHOO YA ZANZIBAR STAZI KATIKA UKUMBI WA MAGEREZA ZANZIBAR.

B
Bahati haikua mbaya sana  au nzuri katika ukumbi wa magereza ambapo hapo ndio ilikua maandalizi ya shoo nzuri kabisa ya zanziba stazi,sikua nyuma mtoto wa maalim kataka maandalizi hayo,kama unavyoona viti ambavyo waliandaliwa washabiki wa zanzibar staz. kunabaadhi ya picha ambazo nimekuekea za wasaniii tofauti tofauti ikiwemo ya zubeda mlamali na ahmed mgeni. nilibahatika kuzungumza na ahmedi mgeni kuhusu nyimbo yake ya sitetereki,kikubwa ambacho alizungumza ahmedi nikuhusu hiyo nyimbo kwamba ndiyo nyimbo yake ya kwanza kutunga katika tasnia ya muziki huu wa taarabu,katka nyimbo hiyo yanazumzwa mengi lkn yy anasema nimaisha ambayo yamemtokea yeye mwenyewe binafsi.
Shoo ilikua nzuri kiasi, kikubwa unachotakiwa nikuwapa saport yakutosha,endelea kfungua blog ya mambo ya zenji utapata kuyajua mengi.

Friday, August 31, 2012

SULTAN KING ATARAJIA KUFUNGA NDOA SEPTEMBA 7

Sultan King bwana harusi mtarajiwa
Hamida Maalim akishow love na bwana harusi mtarajiwa Sultan King
Msanii anaefanya vizuri katika game la muziki wa bongo fleva Zanzibar Sultan King anatarajia kufunga ndoa ijumaa ijayo tarehe 7 mwaka huu na party inatarajiwa kufanyika Salama Hall Bwawani.

MSHINDI WA 3 KATIKA SHINDANO LA BIBI BOMBA AHOJIWA KATIKA NIPE NIKUPE

Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe  leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.

Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)

Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.

Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.

Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.


MANENO HAYO


Tuesday, August 28, 2012

RAHA UTAMU!! ALI NAHODA NDIO YUPO HEWANI MDA HUU

Mtangazaji wa kipindi cha Raha Utamu Ali Nahoda

Kama unasikiliza Coconut Fm 88.2 hapo ulipo utakua unapata burudani ya nyimbo za Taarab za taratibu kidogo kupitia kipindi cha Raha Utamu ambacho ndio kipo hewani mda huu. 

Ali Nahoda ndio anatoa vitu vitamu kwelikweli kupitia mawimbi ya Mambo ya Zenji kila siku ya jumatatu hadi ijumaa.

SIKU NJEMA

Show 5 akiwa na Diva Rayshizzle katika Run the Beat
Show 5 Yoram akiwa ametupia ile mbovu
Rayshizzle na Hamida Maalim
Dj dr B na mwanadada Rayshizzle
Hamida Maalim na Dj Dr B
Diva wa Fleva 145 Rayshizzle (Queen of afternoon showz)

Saturday, August 11, 2012

NDANINYA KIPINDI CHA NIPENIKUPE NIKIWA MIMI HAMIDA MAALIM NA MZEE ISSA AKA SHAROBARO TUMBO.

 Mzee Issa maarufu kama Sharobaro Tumbo akiwa kwenye mahojiano
Hapo unaponiona ni mimi hamida maalim nikiwa na mzee ambae anashiriki mchezo wa husda ambao unaonywesha katika TV yetu ya zanzibar na pia kuutoa katika redio yetu ya COCONUT FM, Ni maarufu kwa jina la Mzee Sharobaro Tumbo,kwenye mchezo wa husda ameshiriki yeye ni mmoja kati ya wanga ambao wanashiriki kutoa watu ambao wanawafatilia katika habari zao hizo, mchezo huo  huutoa katika kipindi cha nipenikupe ambacho hukiendesha HUSNA B AKA mgeni wa bahari, katika kipindi hicho huwa kinamambo mengi mojawapo ni hii segment ya filam zetu huanza saa 4 na nusu asubuhi,na huu mchezo wa husda huutoa kila siku ya ijumaaa, swali  ambalo nilimuuliza mzee sharobarotumbo ,wananchi wanampokeaje anapokutananao mitaani kutokana na ule uhalisia anaocheza katika mchezo huo wa husda?alijibu kwamba wapo wanao muhisi kama ni mchawi kweli na wapo wanao amini kama ule ni mchezo tu na wanaelimisha, mchezo huu utaendlea kuu sikia baada ya mwezi myukufu wa ramadhani,kwasasa tupo kiramadhani zaidi nakutakia ramadhani njema.

Friday, August 10, 2012

h
Leo tukiwa katika kipindi cha nipenikupe ikiwa ni  ramadhani  ya 21 nikiwa mimi Hamida maalim pamoja na thuwaiba jamal,tunajua kwamba huu ni mwezi mtukufu wa ramadhani , kikubwa ambacho tulikizungumzia ni jinsi gani binaadam anatakiwa kuepukana na mambo ambayo yanabatilisha funga yake. pia tulikuwa na ustadhi Muhammed haji akifafanua  kiundani jinsi gani mtu anaweza kuilinda funga yake ili isiweze kubatilika katika nyanja tofauti tofauti kwa mwezi huu mtukufu wa ramadhani,pia shekhe alisisitiza  kwawale ambao wanadhani kua ramadhani ni mchana tu  kwa mujibu wa dini ya kiisilam  huwa wanakosea ,kupitia maelezo ya sheikh huyo tumepata kujifunza mengi ndani ya siku hii ya leo,

Sunday, August 5, 2012

HUYU NDIE MUME WA HUYO MWANAMKE

 
Huyu ndie mume wa huyo mwanamke ambae unaiona pichayake hapo juu, na ndie kewe wa kwanza na wamejaaliwa kuapta nae watoto wa tatu,na toka wamefunga ndoa wameisha timiza miaka mitatu lakini kwa habari ambazo nimezipata kutoka kwenye blog ya dina,nikwamba maisha yao sio mazuri sana,maisha ya mama huyu yamekua ya misukosukona huyu mumewe,mara kapigwa mara kachanwa na viwembe, kuna baadhi ya siku bibi huyu na mumewe,walitofautiana kiswahili kidogo baada ya mumewe kuoa mke wa pili,kilichofuata hapo mume kuelemea kwa mke mpya,kuna siku mke huyo wa kwanza akiwa na shogaake akitembeatembea,mara akatokea mumewe akiwa na gari anaendesha,mume akamwambia mkewe asimame anamazungumzonae,mke akamjibu kwamba siwezi kusimama,hapo ndipo mume akaona bora amvamie kwa gari na kumburuza kwa umbali wa kama mita 150 mpaka alipo fika kwenye tuta ndipo akachomoka na mume kukimbia,kiukweli aliumia sana, alichukuliwa na kukimbizwa hopitalini,maumivu yalikua makali sana kwani aliumia ndani kwa ndani naalivunjia mbavu 7,jitihada zilifanyika lakini ilishindikana kwani aliumia sana,innalilah wa innailaihi rajunna mwanamke huyo amefaiki dunia,wanaume wenye roho hii wanatakiwa kuchukuliwa hatia.

JAMANI HAYA NI MAPENZI KWELI?


 
Hii hali ya unyanyasaji kwa wanawake itaisha lini jamaniiii.

HURUMA KWA MAMA NA MTOTO NI MUHIMU SANA.