Saturday, August 11, 2012

NDANINYA KIPINDI CHA NIPENIKUPE NIKIWA MIMI HAMIDA MAALIM NA MZEE ISSA AKA SHAROBARO TUMBO.

 Mzee Issa maarufu kama Sharobaro Tumbo akiwa kwenye mahojiano
Hapo unaponiona ni mimi hamida maalim nikiwa na mzee ambae anashiriki mchezo wa husda ambao unaonywesha katika TV yetu ya zanzibar na pia kuutoa katika redio yetu ya COCONUT FM, Ni maarufu kwa jina la Mzee Sharobaro Tumbo,kwenye mchezo wa husda ameshiriki yeye ni mmoja kati ya wanga ambao wanashiriki kutoa watu ambao wanawafatilia katika habari zao hizo, mchezo huo  huutoa katika kipindi cha nipenikupe ambacho hukiendesha HUSNA B AKA mgeni wa bahari, katika kipindi hicho huwa kinamambo mengi mojawapo ni hii segment ya filam zetu huanza saa 4 na nusu asubuhi,na huu mchezo wa husda huutoa kila siku ya ijumaaa, swali  ambalo nilimuuliza mzee sharobarotumbo ,wananchi wanampokeaje anapokutananao mitaani kutokana na ule uhalisia anaocheza katika mchezo huo wa husda?alijibu kwamba wapo wanao muhisi kama ni mchawi kweli na wapo wanao amini kama ule ni mchezo tu na wanaelimisha, mchezo huu utaendlea kuu sikia baada ya mwezi myukufu wa ramadhani,kwasasa tupo kiramadhani zaidi nakutakia ramadhani njema.

No comments:

Post a Comment