Thursday, July 26, 2012

MV KALAMA, MV SEPIDEH NA MV SEAGUL ZAFUTIWA HATI YA KUFANYA KAZI ZANZIBAR


Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.

Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.  Endelea hapa

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR NA VIKOSI VYA ULINZI NA TAASISI ZA KIRAIA WAPEWA PONGEZI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mkuu wa Mabalozi wa Nchi za Nje waliopo Tanzania Bwana Juma Alfan Mipango hapo Ofisini kwake Baraza la wawakilishi Mbweni.
Pembani yao ni Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu { UAE } Bw.Mallallah  Mubarak Alameri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  akizungumza na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni wa PPF Bibi Lulu Mengele aliyefika Zanzibar kutoa mkono wa pole kwa niaba ya Uongozi wa Mfuko huo kufuatia ajali ya meli ya hivi karibuni karibu na Kisiwa cha chumbe Zanzibar.
Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni { PPF } Bibi Lulu Mengele akiwasilisha salamu za rambi rambi kwa Makamu wa PILI WA Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kufuatia ajali ya Meli ya M.V.Skagit iliyotokea wiki iliyopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Bishop Michael wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar mara baada ya kuwasilisha salamu zao za rambi rambi hapo ukumbi wa Baraza la wawakilishi Mbweni.
Pembeni ni Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo Bwana Nuhu Sallanya.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na Vikosi vya Ulinzi, pamoja na Taasisi za Kiraia imepongezwa kwa hatua  iliyochukuwa  katika kukabiliana na Maafa yaliyotokea ya kuzama kwa Meli ya M.V. Skagit wiki iliyopita.
Pongezi hizo zimetolewa na Uongozi wa Taasisi tofauti zinazoendelea kutoa mkono wa pole  hapa Zanzibar kufuatia vifo vya watu kadhaa waliokuwemo ndani ya Meli hiyo iliyopata ajali karibu na Kisiwa cha Chumbe.

Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pencheni { PPF } Bibi Lulu Mengele Bishop  Michael wa Kanisa la Anglicana Dayosisi ya Zanzibar pamoja na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu { UAE } Bwana Mallallah Mubarak Alameri wakitoa mkono huo wa pole kwa Balozi Seif walisema hatua hiyo imesaidia kuokoa maisha ya wananchi kadhaa.
Walisema walio wengi wameshuhudia jitihada hizo za uokozi zilizoleta matumaini ndani ya nyoyo za Jamii.

Hata hivyo wawakilishi hao wa taaasisi tofauti walisema licha ya juhudi hizo za Serikali lakini bado ipo haja ya msingi ya kufuatwa kwa sheria na Taratibu sa usafiri wa Baharini.
Walisema utaratibu huo mbali ya kupunguza zinazoweza kuepukwa lakini pia utasaidia kuondosha mwanya kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji wakorofi wanaoendesha biashara hiyo ya vyombo vya usafiri wa Baharini.
“ Kitu cha msingi ni kufuatwa kwa sheria na taratibu za usafiri nah ii itaondosha uzembe na ujanja unaotumiwa na wafanyabiashara wakorofi”. Alisisitiza Balozi wa UAE Bwana Mallallah.

Naye kwa upande wake Bishop Michael wa Kanisa la Anglikana la Mkunazini Dayosisi ya Zanzibar amesema hatua za serikali za kurejesha hali ya amani kufuatia fujo za  baadhi ya Vijana zilizofanywa hivi karibuni imeleta faraja kwa waumini wa kanila lao.
Bishop Michael alisema Uongozi wa Kanisa hilo utaendelea kuwaelimisha Waumini wao kulinda na kuheshimu amani ya Taifa ambayo inahitajiwa na kila mwana Jamii.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Viongozi wa Serikali wanaendelea kupata matumaini kuona Taasisi na mshirika mbali mbali ndani na nje ya Nchi yanaunga mkono juhudi za Serikali.
Balozi Seif alisema Serikali kwa upande wake itaendelea kuchukuwa hatua madhubuti ili kuzuia majanga yanayoweza kuwepukwa ambayo yamo ndani ya uwezo wa mwanaadamu.
“ Tumeanza kuchukuwa hatua za kukabiliana na hali hii kwa kuwaomba washirika wetu ndani na nje ya Nchi kutusaidia katika sekta hii Likiwemo hili zito la upatikanaji wa meli kubwa ya usafirishaji wa wabiria na mizigo”. Alifafanua Balozi Seif.

 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
26/7/2012.
 

SWAUMU YA LEO IMO!!!

Mariam Hamza mtoto wa pili wa bi Hamida Maalim alipokuja kutembelea Coconut Fm leo
Mariam
Hamida Maalim nikiwa na Mama wa mitaani Aisha Omary kushoto tukibadidlishana mawazo kuhusu mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wednesday, July 25, 2012

RAMADHANI KAREEM.....JAMILA ABDALAH

Mwanamke kujistiri huu ndio muonekano wa Baby J kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani tofauti na vile watu walivyomzoea kwa muonekano wa kawaida.

Friday, July 20, 2012

RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR ALI MOHAMED SHEIN AWASISITIZA WAISLAM KUWA WATUMIAJI WAZURI WA MISKITI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, amewasisitiza Waumini wa dini ya Kislamu kutoitumia misikiti kuwa vivutio vya kusababisha uhasama, malumbano au kuwafarakanisha waumini na watu wengine.
 
Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo katika ufunguzi wa msikiti wa Rahmatullah uliopo Mwanyanya, Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, ambapo viomngozi mbali mbali wa dini, vyama na serikali walihudhuria akiwemo Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
 
Katika hotuba yake Dk. Shein alieleza kuwa  misikiti iwe kwa ajili ya ibada pamoja na kuendeleza elemu miongoni mwa waislamu.

KARIBU MGENI WETU RAMADHANI TWAKUKARIBISHA KWA FURAHA NA AMANI SISI KRUU NZIMA YA COCONUT FM KWA PAMOJA AMIN RABIL ALAMINA..

Meneja wa Coconut Fm ambae pia ni mtangazaji wa kipindi cha Nipe Nikupe akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuzungumza na watangazaji wake.
Juu na chini ni picha ya pamoja ya watangazaji wa Coconut fm
Coconut fm yajipanga kufanya vipindi vizuru vitakavyoendana na mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni siku chache zimebaki kuweza kuupokea mwezi huo mtukufu.

Meneja wa Coconut Fm Husna Abdul Megeni wa Bahari alisema "Coconut fm ni redio inayomhudumia vizuri mzanzibari katika kupata taarifa muhimu za ndani na nje na kwa upande wa burudani pia hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kumpatia huduma nzuri zaidi kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani" aliyaesema hayo jana alipokuwa akizungumza na watangazaji wa Coconut fm na kusisitiza kuwa vipindi vimepangwa vizuri kulingana na mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Pia amewataka wasikilizaji wa Coconut fm kuendelea kusikiliza vipindi vizuri vilivyondaliwa kwa ajili ya mwezi mtukufu na kuwahakikishia kuendelea kutoa huduma bora itayokidhi haja yake kwa kipindi chote.

Kwa upande wa wafanyakazi na waendeshaji wa vipindi wamesema wamefurahishwa sana na mpangilio wa vipindi walioupanga kwa ajili ya Ramadhani.

hawa ni watoto ambao waliokolewa baada ya boat hiyo kuzama,inililahi wainnailaii raj una.
 Kijana huyu ni moja yawale ambao wameokoka katika ajali hiyo ya meli ambayo imelikumba taifa
hapo akielezea jinsi gani m,mungu alivyo mjaalia kunusurika.


Thursday, July 12, 2012

Hapo tulipo ni maeneo ya nyuma ya steji kabla Daimond plet nam hajaanza shoo.
hao ni densaz wa plet nam msafi nikishoo nao kabla hajaoyesha vitu vyao.
Jamanii mtoto nilifurahije na vijanaa adi raha yani ful mafuraha yaniiiii.
Aiseeee ni nomaaaa kijana Sultani kingi mtoto kutoka jupiter jinsi alivyo fanya vituuuz

Hapo kijana daimond plet na msafiiii akitoka jasho baada ya kufanya vitu vya hatarii stejini yani we acha tu
Ni tamasha la kumi na tano la ziff ambalo linaendelea  nchini Zanzibar na limepokelewa vizuri sana na wananchi wa Zanzibar, katika tamasha hilo kijana ambae anafanya vizuri sana hapa nchini Tanzania katika muziki wa bongo fleva ,Daimond plet nam msafiii alipata nafasi ya kuwa burudisha wananchi wa zanzibar na wageni (watalii) kabla ya kwenda stejini Daimondi alipata nafasi ya kufanya mahojiano  coconut fm na mtangazaji wa  run the beat Yoram shoo tano, kikubwa alicho ahidi ni kufanya shoo moja kali sana,na baada ya kutinga katika steji kitu ambacho alikifanya huwezi amni, alifanya shoo moja kali sana alitisha mbayaaaa.
Mbali na Daimond, kijana kutoka zanzibar  Sultani king  alifanya shoo ambayo hakuna mtu aliyetarajia kwa kupafom live.

Wednesday, July 11, 2012

KARIBUNI WAGENI WETU

Tumepokea wageni wageni 7 leo kutoka chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Zanzibar na 1 kutoka DSJ, tunafuraha kubwa ya kupata ugeni huo ambao watakuwepo kwa muda wa miezi 2 kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo.

Katika picha ya juu kutoka kushoto ni Said Mohammed kutoka Zjmmc, Saada Khamis kutoka Zjmmc, Mastura Maulid kutoka Zjmmc, Rehema Khamis kutoka DSJ, Mwakaje Khamis kutoka Zjmmc na mwisho ni Rehema Makame kutoka Zjmmc.....endelea hapa

KWA RAHA ZETU TUKISONGESHA NIPE NIKUPE LEO

Mie Hamida Maalim
Aisha Omary mamaa wa mitaani
Joyce Ngerangera
Mie nikiwa na Joyce pamja Aisha

Sunday, July 1, 2012

MIE NIKIWA KATIKA KIPINDI CHA MAMBO YA ZENJI LEO

 Hapa unapo niona nilikua nikipitia sms ya msikilizaji wangu wa mambo ya zenji
Na hapo pia nilikua nikipitia sms ambazo zilitumwa kupitia sm yangu ya mkononi

Maranyingi umezoea kunisikia siku ya jumamosi katika Rusharoho Kitchen part kila siku za juma mosi, lakini leo ilikuwa ni suprise kwako kunisikia katika Mambo ya Zenji kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 3 za usiku, 
Nimekupasha ishu ya Mwanahawa ali na mama wa mipasho nchini Tanzania na Malkia wa mipasho Khadija Omari Kopa kuwa jukwaa moja kesho nitakupasha zaidi.
Ashura Machupa kutoka katika kundi la mashauzi classic na kuamua kuimbia zing zong, na nilimuuliza swali katika kipindi cha kitchen part kwanini aliamua kutoka katika bendi hiyo ya Isha,alicho jibu nikwamba maslai ni madogo ndipo akaamua kutoka,lakini mengi zaidi tembelea blog hiii uta pata na pia endelea kusikiliza rusha roho kitchen part kila jumamosi.