Thursday, June 28, 2012

UKUMBI WA TRAVENTINE JUMAPILI HIII WAKUTANA KHADIJA KOPA NA BIBIE MWANAHAWA ALI.

Malikia wa mipasho au gwiji la mipasho tanzania khadija omari kopa.

Mafahari hawa wawili bibie Mwanahawa ali mama mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni,na malkia wa mipasho Tanzaniabibie Khadija omari kopa,wanatarajia kukutana jukwaa moja ndani ya ukumbi wa traventine hotel katika kutoa burudani ya kufa mtu, ni siku ya jumapili wiki hiii tarehe mosi ya mwezi wa saba, na hapo ndipo tutakapojua nani mkali lakini kwa wewe ambae ni mshabiki wa muziki huu wa taarab  pendelea kutembelea blog hii ya mambo ya zenji utapata kujua mengi zaidi. Mashauzi classic bendi chini ya usimamizi wa thabiti abduli mkono usio igika.
Mama wa sauti ya kumtoa nyoka pangoni bibie mwanahawa ali.


Tuesday, June 26, 2012

UAMSHO WAKANA KUANDAA MAANDAMANO, WAWATAKA WANANCHI KUHUDHURIA KATIKA MAONI YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 

Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiislamu (JUMIKI) imepinga uvumi uliosambazwa nchini kuwa leo kutakuwa na maandamano ya Jumuiya hiyo na kudai kuwa propaganda hizo zinaendeshwa na baadhi ya watendaji katika jeshi la polisi na usalama wa taifa ambao hawaitakii mema Jumuiya yao.

Hayo yamesemwa na Amiri wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid Ahmed wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo ZanzĂ­bar kuhusiana na tuhuma ambazo wamezitoa kwa Jeshi la Polisi dhidi ya Jumuiya yao.

Amedai kuwa Jumuiya haijapanga maandamano kwani ni taasisi inayofanya kazi zake kisheria nakwamba hata ikitokezea kufanya maandamano basi watafuata taratibu zote za kisheria ikiwa ni pamoja na kulitaarifu rasmi Jeshi la Polisi.

Aidha amedai kuwa kuna mkakati wa muda mrefu wa kutaka kuwabatiza viongozi wakuu wa jumuiya hiyo kesi za ugaidi hususan Amir Mkuu wa jumuiya ya Maimamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed ili kuzima vuguvugu la kudai Zanzibar huru.

Shekh Faridi amedai kuwa inasemekana kuna mahusiano makubwa baina ya watendaji ndani ya Jeshi la polisi pamoja na baadhi ya wageni wanaosadikiwa kuwa ni raia wa Marekani juu ya kuutekeleza mkakati huo baada ya kuwa tayari umeshakamilika.

Amedai kuwa kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za kirai ambao umekuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi Zanzibar kwa kuwanyima haki ya kufanya mihadhara yao ndani ya Misikiti  ambapo Juni 17 mwaka huu wananchi mbalimbali walijeruhiwa kwa mabomu katika vijiji vya Donge,Mkwajuni na Mahonda.

Ameliomba Jeshi la Polisi kufanya kazi zake za kulinda usalama wa wananchi na mali zao na kuacha kufanya kinyume chake kwani huko ni kuchochea chuki kati ya Jeshi hilo na raia.

Amesisitiza haja ya wazanzibari kuungana na kuachana na Itikadi zao za kivyama katika kudai hadhi ya Rais na mamlaka ya Nchi ya Zanzibar ndani na nje ya Zanzibar pale tume ya mabadiliko ya Katiba itakapoanza kazi zake.

Kwa upande wake Naibu Naibu Amir Jumuiya Ya Uamsho Na Mihadhara Ya Kiisilam Sheikh, Azan Khalid Hamdan amewaomba wanahabari nao kuwa makini katika taaluma yao kwa kufanya usawa wa taarifa ambazo wamekuwa wakizitoa.

Hivi karibuni Jumuiya hiyo ilitangaza rasmi kushiriki kikamilifu katika zoezi zima la kutoa maoni yao katika mchakato wa kupata Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kubadili msimamo wao wa awali wa kuisusia Tume hiyo.

MWISHO.

IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

26/06/2012

VIDEO YA MADEMU WAZURI KUZINDULIWA VUVUZELA PUB

Kwa mara ya mkali wa muziki wa kizazi kipya kwa commercial style Rico Single ameamua kuzindua video ya ngoma yake mpya ya Mademu Wazuri.
Rico Single ambaye hivi sasa anafanya vizuri sana na ngoma yake ya Mama Africa ambayo amemshirikisha mwanadada Baby J na ngoma ya Wafanyakazi ambayo inamgusa kila mfanyakazi amefunguka kusema kuwa ameamua kuizindua video hiyo ya Mademu wazuri live kwa mashabiki wake kabla hajaiachia kwenye vituo vya TV.
Mademu wazuri ni bonge moja la ngoma ambalo bado hajaiachia kwenye kituo chochote cha redio na bado hajajua lini hasa ataiachia ila kwa sababu yuko na love ya kutosha kwa mafans wake ameamua kula nao bata kupitia video ya ngoma hiyo.
Kwa mara ya kwanza bata.....Cont....

Tuesday, June 19, 2012

KHADIJA KOPA AMUIMBA MWIZI ALIYEIBA GARI LAKE

Mamaa wa kujiamini Tanzania nzima katika tasnia ya muziki wa Taarab wengi wanamuita Malkia  wa mipasho, Khadija Omar Kopa ambae wiki chache zilizopita alikuwa kwenye majonzi makubwa baada ya kuibiwa gari lake aina ya toyota noah na watu wasio julikana.
Hali ambayo imempa funzo kubwa katika maisha yake na kupata wazo la kutunga wimbo wenye mashairi mazuri ya kuelezea namna mjini kunavyoweza kumfunza mtu kama funzo alilopata yeye baada ya kuibiwa gari lake mzigo amabao tayari ameshaurekodi na kuubatiza jina  la Mjini chuo kikuu.
Siku chache zilizopita Bi Khadija ameusambaza wimbo huo ambao umerekodiwa Sound Crafters Studio ya jijini Dar chini ya usimamizi wa Yaniki, katika vituo mbalimbali vya redio na kusema kwamba mashabiki wake wakae tayari kwa video ya wimbo huo.
Katika wimbo huo wa Mjini Chuo Kikuu Malkia Khadija ameamua kumponda kibaka aliyeiba gari lake aina ya Toyota Noah na kumuacha katika hali ya funzo kwa maisha ya mjini..


Friday, June 15, 2012

ISON AGONGA VIDEO YA HALOO BABA

Msanii maarufu mjini Zanzibar aliyekuwa akiigiza kwenye kundi la Black Roots almaaruf kama Mwinchande akicheza party ya Mr President kwenye video ya Haloo baba ya Ison, Mr President akiwa kwenye kikao muhimu na kamati yake pamoja na waandishi wa habari alijikuta akipokea simu kutoka kwa mtoto wake na kusahau kama yupo kwenye kikao muhimu alijikuta........Bonyeza hapa endelea