Tuesday, December 20, 2011

SHANGWE ZA EPIQ NATION NDANI YA VIWANJA VYA KISONGE NOMAAAAAAAAAAAAA!

Baadhi ya mashabiki wa burudani wakizidi kumiminika katika viwanja vya Kisonge, kushuhudia tamasha la EPIQ NATION lililoandaliwa na kampuni ya ZANTEL.
 Ilikuwa hapotoshi kwa kweli.
 MC Abdalla Ambua 'Dullah', akiwajibika katika tamasha hilo, huku umati wa wapenda burudani wakiwa makini kumsikiliza.
 Msanii wa Bongo Flava Mr Blue akitowa burudani katika viwanja vya Kisonge, Michenzani, katika tamasha la EPIQ NATION.
 Piga keleeeeeeeee! mikono juuuuuuuuuuuuuuuu!

Msanii Matonya akifanya vitu vyake katika jukwaa wakati wa  Tamasha la EPIQ NATION katika viwanja vya Kisonge, Michenzani, akitowa  mistari yake.
 Kamata mwizi mennnnnnnn!

Tuesday, December 6, 2011

VIJANA WAWILI WANAOKIMBIZA KIPINDI CHA MAMBO YA ZENJI KINACHOSIKIKA KILA SIKU YA JUMAPILI COCONUT FM!

 Hapa nikiwa na Best wangu wa ukweli Mamaa wa mitaani, Aisha Omar tukifurahi baada ya kumaliza majukumu ya kiofisi ndani ya kipindi cha MAMBO YA ZENI kinachorushwa kila siku za Jumapili hapa hapa mjengoni (88.2 COCONUT FM.
 Usijali ni pozzzzzzzzz tu la kawaida!
Hapa mjengoni ilikuw ni furha baada ya kumaliza kuwajibika.

Saturday, December 3, 2011

USIKU WA 'DINNER' YA ZATUC, ZANZIBAR BEACH RESORT!

 Ilikuwa ni usiku mzuri kweli kwa waliobahatika kuhudhuria katika 'dinner' iliyoandaliwa na ZATUC.
Na mimi nilikuwepo katika chakula cha usiku kilichoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
 
Na huyu naye alikuwepo! Sijui alikwenda kutafuta kitu gani?


Tuesday, November 29, 2011

SAFARI YANGU NI NZURI SANA NA NIMEINJOY KITU CHA HARUSI YA MY BROTHER

Baada ya kupumzika kwa masaa kadhaa pande hizi niliamua sasa kutoka na kwenda kuendelea na mishe za town ila msijali ma fans am on the way back 2 Znz
Hapa nilikuwa nipo kwenye zoezi la kushuka ngazi mwenzangu sio mchezo
Baada ya kufanya zoezi la kushuka ngazi nikaamua kujitia ndani ya lifti

Monday, November 28, 2011

MWENZENU NIPO SAFARINI

Nawamisi sana mashabiki wangu wa Mambo ya zenji na Rusha Roho Kitchen Party wiki hii hamjanisikia katika kipindi coz niko safarini nawenda wote wikiend ijayo mia mia nimejipanga ile mbaya utapata umbea wa niliko sasa mwaaaaaaaaa

Friday, November 4, 2011

MKE WA MAKAMO WA RAIS MGENI RASMI UZINDUZI WA T-MOTO!

Mke wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal.

MKE wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa kundi jipya la Taarab na albam ya kwanza ya kundi hilo, ambalo kwa sasa limekuwa gumzo kubwa kwa mashabiki wa muziki wa Taarab Nchini, Tanzania Modern Taarab (T-Moto) ama Real Madrid.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa kundi hilo, Amini Salmini, alisema kuwa uzinduzi wa kundi hilo ulisogezwa mbele hadi kesho Ijumaa, badala ya tarehe ya kwanza iliyokuwa imepangwa ya oktoba 28, kutokana na ukumbi huo kuwa na shughuli ya ghafla ya Waziri Mkuu katika tarehe hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika uzinduzi huo.
Aidha Amini alisema kuwa baada ya ratiba hizo kuingiliana katika ukumbi huo mmoja wa Diamond Jubilee, ilibidi kundi hilo kusitisha na kusogeza mbele uzinduzi wake ambapo kwa sasa maandalizi yote kuhusu uzinduzi tayari yamekamilika.
Amini alivitaja vikundi vitakavyosindikiza onyesho la uzinduzi huo kuwa ni pamoja na Bendi mahiri inayoundwa na vijana watatu, Mapacha wa3, Bendi kongwe nchini, Msondo Ngoma, Sabaha Salum, anayeimba miondoko ya Taarab pamoja na Kikundi cha Sanaa cha Twins Voice, kinachoimba nyimbo za kuhamasisha kujilinda dhidi ya magonjwa ya Ukimwi.
Pia Amini alitaja viingilio vya onyesho hilo kuwa mashabiki wote wataingi ukumbini kushuhudia onyesho hilo kwa kulipa sh, 10,000 tu, ambapo pia baada ya uzinduzi huo zitapatikana Kanda za albam hiyo zitakazokuwa zikiuzwa ukumbini humo.

Friday, September 23, 2011

KAA MKAO WA KULA KUPITIA BRAND NEW BLOG YA MAMBO YA ZENJI

Mie ndio Hamida Maalim pembeni yangu mama wa mitaani bi Aisha Omary ukisikia wale wakali wa mipasho Zanzibar ndio sie watoto wa kike na bahti zetu upo. Sasa yale yote uyasikiayo kupitia kipindi cha Mambo ya Zenji hapa Coconut Fm sasa utayapata humu bila mchujo