Friday, October 19, 2012

LULU AIBUKA NA SINGLE YAKE

Ni msanii mpya Lakini pia anafanya shughuli za utangazaji kupitia Safari Fm Mtwara Jina Halisi Zakia Lulu Jama Na Jina La Kisanii Ni ELLE,Ngoma yake hii mpya na ya Kwanza amemshirikisha kijana pia anechipukia kimuziki toka Mtwara Pia na Ngoma yenyewe hii imefanyika Mkoani Mtwara Na Producer Geoff Master.......Ni Zouk Moja Nzuri Na Tam Sana....Pata Muda Wa Kusikiliza Uone Utofauti Amezaliwa August 31 Na ukitaka mengi zaidi kujua kutoka kwake mcheki katika Facebook (Lulu Jama)......

FURAHA YANGU YAGEUKA ZAWADI BABY J

WASANII WATATU AKIWEMO ALPHA KUTOKA JUPITER RECORDS, JOBFIRE KUTOKA MK
RECORDS NA ABRAMY KUTOKA APRISE MUSIC WAMEFANYA REMIX YA WIMBO WA BABY J FURAHA YANGU KAMA ZAWADI KWA MWANADADA HUYO AMBAYE KWA SASA ANATARAJIA KUINGIA KATIKA MAISHA YA NDOA.

WAMESEMA KWAMBA KUTOKANA NA KUZIKUBALI SANA KAZI ZA MWANADADA HUYO ANAYEFANYA POA KTK GAME LA MUZIKI WA KIZAZI
KIPYA WAMEPENDA KUMZAWADIA WIMBO HUO WA FURAHA YANGU KAMA KUMPONGEZA KWA MAAMUZI YA BUSARA ALIYOYAFANYA KWA KUAMUA KUWA TAYARI KUINGIA KATIKA HARAKATI ZA KUELEKEA KWENYE MAISHA YA MUME NA MKE JAMBO AMBALO NI LA BUSARA NA HEKIMA KTK MAISHA. WANAMTAKIA KILA LA KHERI MWANADADA JAMILA ABDALLAH A.K.A BABY J KTK SAFARI YAKE YA KUELEKEA KTK MAISHA YA NDOA. TUNAMPENDA SANA NA KUMJALI DADA YETU NA PIA TWAZIPENDA KAZI ZAKE.

MZIGO MPYA AACHIA QUEEN DARLEEN

Mwanadada Queen Darleen aachia Ngoma Mpya inaitwa KOKORO......Imefanywa Na Producer Tuddy Thomas.....Video Inafanywa Wiki Hii Na Adam Juma (Visual Lab Next Level)
Hii Ni Ngoma Yake Ya 5 Tokea Ameanza Kufanya Mziki Mwaka 2000 Ya Kwanza Ilikuwa Wajua Ft. Alikiba, Ya Pili Ilikuwa Cheza Nami Ft. Kgt, Ya 3 Ilikuwa Ilikuwa Kupendapenda Ft. Sho daddy, Ya 4 Ilikuwa Maneno Maneno Ft. Dully Sykes Na Ilifanikiwa Kuchukua Tuzo Ya Best Dancehall/Ragga Kupitia Kili Awardz 2011-2012 Na Kokoro Ndio Single Ya 5.