Friday, August 31, 2012

SULTAN KING ATARAJIA KUFUNGA NDOA SEPTEMBA 7

Sultan King bwana harusi mtarajiwa
Hamida Maalim akishow love na bwana harusi mtarajiwa Sultan King
Msanii anaefanya vizuri katika game la muziki wa bongo fleva Zanzibar Sultan King anatarajia kufunga ndoa ijumaa ijayo tarehe 7 mwaka huu na party inatarajiwa kufanyika Salama Hall Bwawani.

MSHINDI WA 3 KATIKA SHINDANO LA BIBI BOMBA AHOJIWA KATIKA NIPE NIKUPE

Mtangazaji wa kipindi cha Nipe nikupe Husna B
Bi Nasra mshindi wa 3 katika shindano la BIBI BOMBA
Bibi Bomba mshindi wa 3 Bi Nasra akihojiwa na Husna B kwenye kipindi cha Nipe Nikupe  leo akieleza namna shindano lilivyokuwenda mpaka kupatikana mshindi.
Bi Nasra akishow love na Hamida Maalim mara baada ya kumaliza mahojiano yake.

Mzanzibari aliyeshiriki shindano la Bibi Bomba Bi Nasra linalosimamiwa na Clouds TV na Clouds Fm Jijini Dar es Salaam amerejea Zanzibar akiwa amebahatika kuwa mshindi namba 3 na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni moja na nusu taslim (1,500,000/-)

Bi Nasra maarufu kama Bi Naa alieleza changamoto alizokutana nazo kwa kipindi chote walichokuwa katika nyumba maalum waliokuwa wanaishi na kuibatiza jina la Jumba la Dhahabu kutokana na kukamilika kwa mahitaji yote waliyokuwa wakiyahitaji katika nyumba hiyo.
Alisema walikuwa wakishiriki kwenye michezo na mambo mbalimbali waliohitajika kuyafanya ikiwemo kucheza ngoma, mchezo wa kucheza na Nyoka, kupika na kusuka mikeka.

Katika michezo hiyo ipo michezo ambayo aliweza kushiriki ipasavyo na ipo michezo ambayo hakuweza kushiriki kabisa ikiwa ni kucheza ngoma pamoja na kucheza na nyoka.

Bi Nasra anawashukuru wazanzibari wote na watanzania kiujumla kwa kuweza kumpigia kura na kumpelekea kuweza kuwa mshindi namba 3 katika shindano hilo, pia ametoa wito kwa wazanzibari kuweza kushiriki shindano hilo kwa wakati ujao kwani shindano ni zuri na linachangamoto kubwa kwa watu wenye umri kama wake.


MANENO HAYO


Tuesday, August 28, 2012

RAHA UTAMU!! ALI NAHODA NDIO YUPO HEWANI MDA HUU

Mtangazaji wa kipindi cha Raha Utamu Ali Nahoda

Kama unasikiliza Coconut Fm 88.2 hapo ulipo utakua unapata burudani ya nyimbo za Taarab za taratibu kidogo kupitia kipindi cha Raha Utamu ambacho ndio kipo hewani mda huu. 

Ali Nahoda ndio anatoa vitu vitamu kwelikweli kupitia mawimbi ya Mambo ya Zenji kila siku ya jumatatu hadi ijumaa.

SIKU NJEMA

Show 5 akiwa na Diva Rayshizzle katika Run the Beat
Show 5 Yoram akiwa ametupia ile mbovu
Rayshizzle na Hamida Maalim
Dj dr B na mwanadada Rayshizzle
Hamida Maalim na Dj Dr B
Diva wa Fleva 145 Rayshizzle (Queen of afternoon showz)

Saturday, August 11, 2012

NDANINYA KIPINDI CHA NIPENIKUPE NIKIWA MIMI HAMIDA MAALIM NA MZEE ISSA AKA SHAROBARO TUMBO.

 Mzee Issa maarufu kama Sharobaro Tumbo akiwa kwenye mahojiano
Hapo unaponiona ni mimi hamida maalim nikiwa na mzee ambae anashiriki mchezo wa husda ambao unaonywesha katika TV yetu ya zanzibar na pia kuutoa katika redio yetu ya COCONUT FM, Ni maarufu kwa jina la Mzee Sharobaro Tumbo,kwenye mchezo wa husda ameshiriki yeye ni mmoja kati ya wanga ambao wanashiriki kutoa watu ambao wanawafatilia katika habari zao hizo, mchezo huo  huutoa katika kipindi cha nipenikupe ambacho hukiendesha HUSNA B AKA mgeni wa bahari, katika kipindi hicho huwa kinamambo mengi mojawapo ni hii segment ya filam zetu huanza saa 4 na nusu asubuhi,na huu mchezo wa husda huutoa kila siku ya ijumaaa, swali  ambalo nilimuuliza mzee sharobarotumbo ,wananchi wanampokeaje anapokutananao mitaani kutokana na ule uhalisia anaocheza katika mchezo huo wa husda?alijibu kwamba wapo wanao muhisi kama ni mchawi kweli na wapo wanao amini kama ule ni mchezo tu na wanaelimisha, mchezo huu utaendlea kuu sikia baada ya mwezi myukufu wa ramadhani,kwasasa tupo kiramadhani zaidi nakutakia ramadhani njema.

Friday, August 10, 2012

h
Leo tukiwa katika kipindi cha nipenikupe ikiwa ni  ramadhani  ya 21 nikiwa mimi Hamida maalim pamoja na thuwaiba jamal,tunajua kwamba huu ni mwezi mtukufu wa ramadhani , kikubwa ambacho tulikizungumzia ni jinsi gani binaadam anatakiwa kuepukana na mambo ambayo yanabatilisha funga yake. pia tulikuwa na ustadhi Muhammed haji akifafanua  kiundani jinsi gani mtu anaweza kuilinda funga yake ili isiweze kubatilika katika nyanja tofauti tofauti kwa mwezi huu mtukufu wa ramadhani,pia shekhe alisisitiza  kwawale ambao wanadhani kua ramadhani ni mchana tu  kwa mujibu wa dini ya kiisilam  huwa wanakosea ,kupitia maelezo ya sheikh huyo tumepata kujifunza mengi ndani ya siku hii ya leo,

Sunday, August 5, 2012

HUYU NDIE MUME WA HUYO MWANAMKE

 
Huyu ndie mume wa huyo mwanamke ambae unaiona pichayake hapo juu, na ndie kewe wa kwanza na wamejaaliwa kuapta nae watoto wa tatu,na toka wamefunga ndoa wameisha timiza miaka mitatu lakini kwa habari ambazo nimezipata kutoka kwenye blog ya dina,nikwamba maisha yao sio mazuri sana,maisha ya mama huyu yamekua ya misukosukona huyu mumewe,mara kapigwa mara kachanwa na viwembe, kuna baadhi ya siku bibi huyu na mumewe,walitofautiana kiswahili kidogo baada ya mumewe kuoa mke wa pili,kilichofuata hapo mume kuelemea kwa mke mpya,kuna siku mke huyo wa kwanza akiwa na shogaake akitembeatembea,mara akatokea mumewe akiwa na gari anaendesha,mume akamwambia mkewe asimame anamazungumzonae,mke akamjibu kwamba siwezi kusimama,hapo ndipo mume akaona bora amvamie kwa gari na kumburuza kwa umbali wa kama mita 150 mpaka alipo fika kwenye tuta ndipo akachomoka na mume kukimbia,kiukweli aliumia sana, alichukuliwa na kukimbizwa hopitalini,maumivu yalikua makali sana kwani aliumia ndani kwa ndani naalivunjia mbavu 7,jitihada zilifanyika lakini ilishindikana kwani aliumia sana,innalilah wa innailaihi rajunna mwanamke huyo amefaiki dunia,wanaume wenye roho hii wanatakiwa kuchukuliwa hatia.

JAMANI HAYA NI MAPENZI KWELI?


 
Hii hali ya unyanyasaji kwa wanawake itaisha lini jamaniiii.

HURUMA KWA MAMA NA MTOTO NI MUHIMU SANA.