Tuesday, June 19, 2012

KHADIJA KOPA AMUIMBA MWIZI ALIYEIBA GARI LAKE

Mamaa wa kujiamini Tanzania nzima katika tasnia ya muziki wa Taarab wengi wanamuita Malkia  wa mipasho, Khadija Omar Kopa ambae wiki chache zilizopita alikuwa kwenye majonzi makubwa baada ya kuibiwa gari lake aina ya toyota noah na watu wasio julikana.
Hali ambayo imempa funzo kubwa katika maisha yake na kupata wazo la kutunga wimbo wenye mashairi mazuri ya kuelezea namna mjini kunavyoweza kumfunza mtu kama funzo alilopata yeye baada ya kuibiwa gari lake mzigo amabao tayari ameshaurekodi na kuubatiza jina  la Mjini chuo kikuu.
Siku chache zilizopita Bi Khadija ameusambaza wimbo huo ambao umerekodiwa Sound Crafters Studio ya jijini Dar chini ya usimamizi wa Yaniki, katika vituo mbalimbali vya redio na kusema kwamba mashabiki wake wakae tayari kwa video ya wimbo huo.
Katika wimbo huo wa Mjini Chuo Kikuu Malkia Khadija ameamua kumponda kibaka aliyeiba gari lake aina ya Toyota Noah na kumuacha katika hali ya funzo kwa maisha ya mjini..


No comments:

Post a Comment